Please send your suggestions to uswahili@aol.com

Wednesday, March 24, 2010

foleni za kwenda bafuni

We ni mswahili pale upangapo foleni za kwenda bafuni kuoga kwenye nyumba za kupanga. Wababa/Washkaji kusimama nje ya bafu wanasubiri utoke huku na miswaki yao mdomoni na hapo hapo wanajadili yanga, simba, arsenal, man etc ilivolala jana ilhali wengine hawana hata TV, kumbe walicheki kupitia dirisha, jirani, bar etc!

7 comments:

 1. Uswahilini. Nimewasili. Nimewasili NYUMBANI maana nami ni mswahili. Nashukuru saana kwa kuniongeza kwenye Facebook na nilipotembekea ukurasa wako nikakutana na hii.
  Nimefurahi kuona nawe unaendeleza kazi njema ya ku-Blog.
  Basi karibu CHANGAMOTONI kusaidiana kuelimisha, kuburudisha, kufunza na kuisaidia jamii.
  Blessings

  ReplyDelete
 2. KARIBU......http://jukwaahuru.com/

  ReplyDelete
 3. Kwa vile nami ni mswahili nimeona si mbaya nikichangia kidogo. Nawe karibu MAISHA NA MAFANIKIO. Hapo konaniiii!!

  ReplyDelete
 4. Siku ukihamia kwenye nyumba ambayo bafu lipo kwa ndani (self contained) na hakuna foleni lazima upakumbuke huku maana utakuwa unakosa stori
  SWALI inakuwaje jamaa wanasubiri kwa nje na wewe uko bafuni/chooni na unaendesha tena kwa sauti watu wote wanasikia, maana mabafu haya ni choo pia, halafu mengi ni ya shimo halafu .........

  ReplyDelete
 5. Lakini mimi sipendi vitu vibaya au maisha ya shida yakaitwa ya `waswahili' kwasababu tunakitia madoa kiswahili chetu!

  ReplyDelete
 6. mwenye blog,she's typical mswahili

  ReplyDelete
 7. What's up, all the time i used to check web site posts here early in the break of day, as i enjoy to find out more and more.

  Also visit my site atlaslm.com

  ReplyDelete